Uchakataji wa matokeo ya wanafunzi katika Mitihani ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa kwa shule za Msingi unategemea kutumia lahajedwali (spreadsheet) au uchakataji wa mikono unaosababisha:
Faili moja ya lahajedwali haiwezi kufunguliwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja. Hivyo, mtu mmoja akitumia, wengine wanasubiri — hii inachelewesha kazi.
Ukokotoaji wa alama kwa mikono huweza kusababisha makosa kama kujumlisha vibaya, kupata wastani usio sahihi, au kuandika namba isiyo sahihi. Hii inaweza kupelekea wanafunzi kupata madaraja yasiyo sahihi.
Kipindi Baraza la Mitihani Tanzania likitangaza matokeo walimu hufanya uchambuzi wa madaraja ya ufaulu wa somo kwa njia ngumu ya kuhesabu na kujumlisha idadi ya wanafunzi wenye ufaulu kwa kila daraja (A,B,C,D,E). Mchakato huu unachukua muda mrefu na wakati mwingine hufanyika kimakosa na kupelekea takwimu zisizosahihi.
Wakati wa kuhamisha alama kutoka karatasi kwenda kwenye kompyuta, mtu anaweza kuchapa namba isiyo sahihi. Mfano: 3O badala ya 30. Kosa dogo kama hili linaweza kubadilisha matokeo ya mwanafunzi kabisa.
Walimu na wasimamizi hutumia muda mwingi kukokotoa alama, kuandaa ripoti za wanafunzi mmoja mmoja, na kukusanya ripoti za ufaulu wa darasa zima. Muda huu ungeweza kutumika kufundisha na kuandalia vipindi vya masomo.
Kumbukumbu za karatasi zinaweza kuharibika, kupotea, au kuharibika kwa maji au moto. Pia ni vigumu kupata data ya miaka iliyopita, na hakuna mfumo wa kuhifadhi nakala (backup) endapo kutatokea janga.
Kuandaa ripoti kwa mikono huchukua muda mrefu na mara nyingi ripoti hazifanani kwa muundo kati ya madarasa au mihula. Pia kuna ucheleweshaji wa kutoa matokeo, na ni vigumu kuzalisha ripoti maalum za uchambuzi wa ufaulu.
Changamoto hizi zote zinaonyesha umuhimu wa mfumo wa kidigitali wa kuchakata na kusimamia matokeo ya wanafunzi katika Mitihani mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi Mkoa — mfumo ambao hupunguza makosa, huokoa muda, na hurahisisha upatikanaji wa taarifa, pia kurahisisha uchambuzi wa Madaraja ya Ufaulu katika Matokeo ya Mitihani ya Kitaifa darasa la nne na saba kwa dakika 1-3 tu.
Matokeo yanachakatwa papo hapo — kutoka siku kadhaa hadi Dakika chache. Uchambuzi wa NECTA kwa dakika 1–3.
Hakuna makosa ya kibinadamu, fomula zinazoharibika, au kuchapa vibaya. Mfumo hukataa alama zisizo sahihi.
Shule, Kata, Halmashauri, na Mkoa — kila ngazi inaona data inayohusika kwa wakati mmoja.
Wazazi/walezi hupokea matokeo ya watoto wao moja kwa moja kwenye simu — bila kuuliza shuleni.
Madaraja A–E, ufaulu wa jumla na somo moja moja, ripoti za Excel na PDF — zote kiotomatiki.
Encryption ya SSL/TLS, backup za kila siku, na seva zenye uptime ya 99%+.
Mfumo una uwezo wa kutenngeneza Fomu ya Mahudhurio.
Mfumo unatengeneza Mpangilio wa Ukaaji wa Watahiniwa katika Chumba cha Mtihani.
| Njia ya Zamani (Excel / Mkono) | Mfumo wa PSRPMS |
|---|---|
| Siku kadhaa hadi wiki za kuchakata matokeo | Uchakataji papo hapo baada ya alama kuingizwa |
| Makosa ya kibinadamu na fomula zinazoharibika | Hesabu za kiotomatiki na Usahihi wa 100% |
| Ugumu wa kukusanya data shule kwenda mkoa | Mfumo wa kati ambapo kila ngazi inaona data |
| Hakuna mawasiliano ya haraka ya matokeo | SMS za matokeo zinatumwa moja kwa moja kwa wazazi |
Hakuna makosa ya hesabu au fomula potofu. Mfumo hufanya kila kitu kiotomatiki na kukataa alama zisizo sahihi.
Inafanya kazi 24/7. Inabadilisha kazi za wiki nzima za walimu kuwa kazi ya saa chache tu.
Huondoa haja ya wazazi kwenda shuleni kuuliza matokeo. Wanapata ripoti kiganjani mwao moja kwa moja.
Mfumo unavuta taarifa moja kwa moja kutoka NECTA. Inachambua madaraja (A–E) kwa Jinsi za Wanafunzi kwenye Ufaulu wa Jumla na Ufaulu wa Somo Moja moja na kuandaa faili la Excel na PDF.
Mwenendo wa ufaulu wa halmashauri zote.
Kulinganisha ufaulu wa shule zote, kubaini shule bora na zenye changamoto.
Ufaulu wa darasa, somo, na nafasi ya shule kwenye kata/halmashauri.
Wazazi hupokea alama za mtoto na nafasi yake darasani mara tu uchakataji unapokamilika.
Huokoa gharama na muda wa shule kuandika na kuchapisha barua za matokeo.
Huondoa msongamano wa wazazi wanaokuja shuleni kuulizia maendeleo ya watoto.
Data zote zinalindwa kwa teknolojia ya SSL/TLS zinaposafiri mtandaoni.
Mfumo unahifadhi nakala (backup) kila siku kuzuia upotevu wa data za shule.
Mfumo haukubali alama chini ya 0 au zaidi ya 50, na hukumbusha ikiwa mwanafunzi amerukwa.
Seva zenye uwezo mkubwa zinahakikisha mfumo upo hewani kwa zaidi ya 99%.
| Mtumiaji | Anaweza Kufanya ✔ | Hana Ruhusa ❌ |
|---|---|---|
| Mwalimu wa Taaluma | Kuingiza alama za mtihani na kuona ripoti za darasa. | Kusajili wanafunzi au kuona shule nyingine. |
| Mkuu wa Shule | Kusajili shule, walimu, wanafunzi, na kuona matokeo ya shule yake. | Kubadilisha matokeo ya shule nyingine. |
| Afisa Elimu (Kata/Halmashauri/Mkoa) | Kuona matokeo ya ngazi yake yote, kulinganisha shule, na kutoa ripoti. | Kuingiza au kubadilisha alama za wanafunzi binafsi. |
kwa kuondoa makosa ya Excel, kuhakikisha usahihi wa data, na kuwashirikisha wazazi kwa ufanisi. Kuanzia Januari 2026, huu ni mfumo wako wa kisasa na salama.
Je, shule yako tayari imesajiliwa?
Timu ya Msaada (Inapatikana muda wowote)
Nawashukuru wote kwa ushirikiano wenu, muda wenu, na kwa kunisikiliza kwa makini katika uwasilishaji huu wa Mfumo wa PSRPMS. Ni matumaini yangu kwamba mmeona umuhimu na faida za mfumo huu kwa shule zetu za Msingi.
Tuonane tena katika hatua zijazo za mageuzi ya elimu yetu. Kwa pamoja, tutafanikiwa.
KWAHERINI! MUNGU AWABARIKI NYOTE.